Tel: +254 (020) 7807600
Email: kerra@kerra.go.ke
Language:

Google Translate Widget by Infofru

Author Site Reviewresults

Tuesday, 07 April 2020

DIBAJI
Mkataba huu wa huduma kwa wateja ni maelezo kuhusu nia ya Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) kutoa huduma bora zaidi kwa wateja na washika dau

MAONO YETU
Kuwa mtoa huduma wa barabara za vijiji zilizo bora, zenye usalama, za kutosha, na zenye ufanisi .

WITO WETU
Kuendeleza, kujenga, kukarabati na kusimamia barabara za vijiji ili kuleta maendeleo ya kijamii, ya kiuchumi, na ya kudumu.


MAADILI YETU
Kama Taasisi ya umma, tumejitolea kutoa huduma za hali ya utalaamu wa juu kwa wateja wetu. Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi unafuata maadili yafuatayo:

 • Uadilifu
 • Utaalam
 • Uongozi
 • Ubinifu
 • Utendaji kazi wa pamoja
 • Uaminifu kwa kutoa huduma
 • Uwakili wa mazingira na wa kiijamii

TUMEJITOLEA:
Kujenga, kukarabati, na kusimamia barabara za vijiji tukitumia fedha zilizotengwa;
Kuwasiliana na washirika kuhakikisha kwamba ujenzi na ukarabati wa barabara za vijiji umetekelezwa kwa haraka iwezekanavyo;
Kutotumia mashine mahala ambapo ajira za mkono zita kamilisha lengo, na kuhusisha wafanyi biashara wetu iwezekanavyo ;
Kuongeza na kueneza uwezo kwa kuwezesha elimu ya wakandarasi na wataalam wa kuajiriwa ;
Kutoa malipo ya madai halali ndani ya siku thelathini (30) tangu kupokea hati sahihi ya madai, na kuthibitshwa na kamati za kupokea, ama vile mikataba kati yetu na wauzaji wa bidha na huduma zinavosisitiza

Fuata mikataba yetu;
Tumia taarifa za mrejesho kama funzo na nafasi ya kuboresha huduma zetu; Karibisha malalamishi yenu na kuyatatua;

Kutoka jumatatu hadi ijumaa, tuta shughulikia umma kutoka saa mbili za asubuhi mpaka saa saba, na kutoka saa nane mpaka saa kumi na moja za jioni, , isipokuwa siku za likizo.
Kukiri kupokea barua pepe ndani ya masaa ishirini na nne, ikitegemea mtandao wa internet kuweko;
Kushughulikia na kuhifadhi taarifa za wateja kwa usiri.

Wajibu wa Mteja
Kuheshimu watumishi wa Taasisi, taratibu na kanuni zilipo;
Kutopotosha watumishi wa Taasisi na rushwa;
Kutowa mawasiliano ya wazi ili kuwezesha watumishi wa taasisi kutoa huduma bora;
Kuto haribu njia nyembamba au njia pande za barabara kwa kuendesha au kusimamisha magari hapo;
Kuto panga mizigo juu ya magari kuzidi kiwango cha uzito uliyokubalika;
Kuto endeleza mpaka ya rizavi ya barabara za vijiji au kujenga miundo isiyo halali hapo
Kutozuia mifreji ya maji bonde iloyo jengwa pande ya barabara za vijiji ;
Kutofunga barabara za vijiji na vijia kwa kuweka maonyesho ya kibiashara au vizuizi vingene
Malalamiko, taarifa ya mrejesho, na maoni
Tunakaribisha taarifa ya mrejesho, malalamiko, utambulisho na maoni kuhusu uboreshaji wa huduma zetu. Mawasiliano yanaweza kufanywa kwa njia ya simu, kinakilishi, barua, au barua pepe kwa anuani zifuatazo:

 

Mkurugenzi Mkuu,
Kenya Rural Roads Authority
S.L.P. 48151-00100
NAIROBI

Simu: +254 -020-8013846/2710464
Kinakilishi: +254-20-4451866
Barua Pepe : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Tovuti: www.kerra.go.ke

Au:
Menaja, Mawasiliano na Uhusiano Mwema
Simu: +254 -020-8013846

Contact Us

Our Head Office

Kenya Rural Roads Authority,
Barabara Plaza, Block B
Airport South Road, Opp. KCAA
P.o. Box 48151-00100,
Nairobi. Kenya

Email: kerra@kerra.go.ke / dgkerra@kerra.go.ke 
Tel: +254 (020) 7807600-05
Mobile: +254 724 735 568

 

 

Our Services

Do you like our services?
 • Votes: (0%)
 • Votes: (0%)
 • Votes: (0%)
 • Votes: (0%)
 • Votes: (0%)
Total Votes:
First Vote:
Last Vote:
Copyright © 2020 Kenya Rural Roads Authority (KeRRA is ISO 9001:2008 Certified). All Rights Reserved.
Joomla! is Free Software released under the GNU General Public License.